IQNA

Fikra za Kiislamu

Fahamu Umuhimu wa Misikiti katika Uislamu

22:01 - September 30, 2022
Habari ID: 3475860
TEHRAN (IQNA) – Misikiti ina nafasi maalum katika Uislamu. Misikiti sio tu ni sehemu za ibada au Sala bali pia ina kazi mbalimbali za kidini, kijamii na kisiasa.

Neno msikiti limetajwa katika Qur’ani Tukufu mara 28, mara 22 katika hali ya umoja na mara 6 kwa wingi.

Katika aya hizi, kuna marejeo ya umuhimu wa misikiti katika Uislamu, baadhi ya kanuni za kidini kuhusu misikiti, Msikiti Mkuu wa Makka, Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds na msikiti wa Al-Kahf (Watu wa Pango).

Misikiti inaitwa nyumba za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo, kinachofanyika msikitini lazima kiwiane na kumdhukuru Mwenyezi Mungu: “Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.” Qur’ani Tukufu Surah Al-Jinn, Aya ya 18)

Kwa kuzingatia aya za Quran na Hadithi, Kaaba huko Makka ni mahali pa kwanza pa kumwabudu Mungu Mmoja na kitovu cha tauhidi: “Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka (jina jingine la Makka), iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.” (Surah Al-Imran, Aya ya 96)

Kwa kuzingatia umuhimu na fadhila za misikiti, Mwenyezi Mungu ameinasibisha misikiti kwa nafsi yake. Ni ishara na inaonyesha umuhimu ambao Mungu anaambatanisha na maeneo haya ya ibada. Kwa hivyo, kinachofanywa ni misikiti inalingana na anachotaka Mwenyezi Mungu na ndani ya masilahi ya Waislamu.

Katika kitabu Kashf al-Asrar (Kufichuliwa kwa Siri), mwandishi Abulfazl Rashideddin Meybodi anasema kwamba msikiti ni nyumba za Mungu duniani. Misikiti inang'aa kwa walio mbinguni kama vile nyota zinavyowaangazia walio juu ya ardhi.

Kwa hivyo misikiti ni sehemu takatifu za Imani, Taqwa (kumcha Mungu), kumwabudu Mwenyezi Mungu, na kuswali. Hata hivyo, madhalimu wanaichukulia misikiti kuwa ni tishio kwao kwa sababu maeneo hayo ya ibada siku zote yamekuwa msingi wa umoja na maelewano na kupiga vita dhulma na ufisadi.

Mwenyezi Mungu amewataja wale wanaowazuia watu wasiende misikitini au kuharibu misikiti kuwa ni watu madhalimu zaidi: “Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.” (Surah Al-Baqarah, Aya ya 114)

captcha