IQNA

Arbaeen ya Imam Hussein AS

Wafanyaziara kutoka nchi 80 washiriki katika matembezi ya Arbaeen

20:20 - September 16, 2022
Habari ID: 3475792
TEHRAN (IQNA)- Gavana wa Karbala, Iraq ametangaza kuwa, wafanyaziara kutoka nchi 80 katika maadhimisho ya mwaka huu za Arbaeen mwaka huu wa 1444 Hijria Qamari sawa na 2022 Miladia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Gavana wa Karbala Ali Al-Miyali alisema “Wafanyaziara  kutoka nchi 80 wameshiriki katika matembezi ya mwaka huu ya Arbaeen.”

Ameongeza kuwa: Mashirika ya serikali ya Iraq na maeneo matakatifu ya Imam Hussein AS na Hadhrt Abbas AS, washiriki Wairaqi na wakaazi wa mji mtakatifu wa Karbala, walitumia uwezo wao wote kuwahudumia wafanyaziara wa Imam Hussein AS ikiwemo usafiri, chakula, huduma za afya na simu bila malipo n.k.

Naibu gavana wa pili wa Karbala alisema: “Tangu siku ya kwanza ya Muharram hadi tarehe 18 Safar, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kukiuka usalama wa Iraq, jambo ambalo linaashiria juhudi za kiusalama na umakini wa vikosi vya usalama.”

Kuhakikisha usalama na afya za mahujaji

Kwa upande mwingine, Nafee Al-Mousavi, Mkuu wa Idara ya Bain al Haramin yenye mafungamano na Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas, alisema: Kuhakikisha usalama na afya ya mahujaji ni moja ya vipaumbele vya idara hii, na katika suala hili, kuna kiwango cha juu cha uratibu wa usalama na vyombo mbalimbali vya usalama katika mji wa Karbala.

Sala za pamoja za jamaa njiani kutoka Najaf kwenda Karbala

Kwa upande mwingine, Sala ya Ijumaa iliyounganishwa ilifanyika chini ya uongozi wa "Syed Ahmad Ashkouri" katika kona ya 208 ya Tariq al-Za'areen (njia ya waenda kwa miguu kutoka Najaf hadi Karbala). Pia wafanyaziara wanasali sala za Jamaa wakiwa wanatembea kwa migudd kutoka Najaf hadi Karbala yenye umbali wa kilomita takribani 70.

تازه‌های اخبار اربعین؛ از مشارکت زائران 80 کشور تا نماز جماعت یکپارچه در طریق الحسین(ع)

Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya habari ya Astan Alavi, Seyyed Ahmad Ashkouri alisema: "Tuliona wazi kwamba wafanyaziara waheshimiwa wana nia ya kuswali kwa wakati, na pia wana nia ya kusali sala ya jamaa, na hii ni dalili nzuri ya Ziara ya Arbaeen.

Mwakilishi wa Wakristo wa Orthodox

Halikadhalika Rogelio Sáez Carbó mwakilishi wa Wakristo wa Orthodox nchini Uhispania na Ureno, akifuatana na "Moussa Al-Aasim", mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Al-Bayt (A.S.), alitembelea Haram Takatifu ya Imam Ali AS mjini Najaf Ashraf.

تازه‌های اخبار اربعین؛ از مشارکت زائران 80 کشور تا نماز جماعت یکپارچه در طریق الحسین(ع)

Akiwa hapo alikutana na "Sayed Isa Al-Khursan", Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali AS na wamejadiliana juu ya masuala ya kibinadamu kati ya dini na kuimarisha uhusiano na kuheshimiana kati ya ubinadamu bila kujali dini, rangi na kabila.

Mwakilishi wa Wakristo wa Orthodox nchini Uhispania na Ureno alionyesha zaidi kushangazwa kwake na huduma za Haram ya Imam Ali AS na Mawakib Hosseini kwa mahujaji wa Arbaeen na akasifu roho ya upendo kati ya wafanyaziara na walinzi wa haram  takatifu kote Iraq.

Shughuli za vituo vya Qur’ani katika matembezi ya Arbaeen

Kwa mujibu wa taarifa ya IQNA kutoka Iraq; kuna mradi maalum wa kusahihisha usomaji wa Qur’ani kwa wafanyaziara wa Arbaeen, unaotekelezwa na  Dar Al-Qur'an ambayo inafungamana na Haram Tukufu ya Imam Ali (AS).

تازه‌های اخبار اربعین؛ از مشارکت زائران 80 کشور تا نماز جماعت یکپارچه در طریق الحسین(ع)

Amir Kassar, mkuu wa tawi la Dar Al-Qur'an amefafanua kuhusu mradi huo na kusema: Vituo 80 vya Qur'ani vyenye wakufunzi na walimu wa Qur'ani wanaume na wanawake zaidi ya 350 vilianzishwa katika mikoa tofauti ya Iraq kwa mnasaba wa Arbaeen Hussaini.

Ufafanuzi wa Arbaeen

Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo mane yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya mwandamo wa Kiislamu na mwaka huu inasadifiana na 17 Septemba.

Baada ya kufa shahidi Imam Hussein (AS) mikononi mwa katili Yazid bin Muawiya, watu ambao walishangazwa na ukatili wa ukoo wa Ummaya walianza kuzuru kaburi lake kutoa heshima zao.

4085956

captcha