IQNA

Uuungaji mkono Palestina

Wananchi wa Iran waandamana kulaani jinai Israel dhidi ya Wapalestina Gaza

19:06 - August 10, 2022
Habari ID: 3475605
IQNA (TEHRAN )- Wananchi wa Iran jana Jumanne walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua shahidi wanawake na watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.

Maelfu ya waandamanaji walioshiriki kwenye maandamano hayo walikusanyika katika Medani ya Palestina jijini Tehran, karibu na ubalozi wa Palestina hapa nchini, huku wakiwa wamebeba bendera za Palestina na makundi ya muqawama.

Aidha waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe za kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza wasio na ulinzi.

Waandamanaji hao walisikika wakipiga nara za 'Mauti kwa Israel', 'Mauti kwa Wazayuni' na 'Mauti kwa Uingereza' huku wakitangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.

Akiuhutubia umati mkubwa wa waandamanaji hao, Khalid Qaddoumi, Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema, "Maadui Wazayuni ambao wamewaua raia wasio na hatia, wanapaswa kushtakiwa katika mahakama za kimataifa za haki za binadamu, na wapewe adhabu kali."

 
 

3480033

captcha