IQNA

Jinai dhidi ya Waislamu

Jeshi la Nigeria lashambulia Waislamu katika maombolezo ya Imam Hussein AS, watu kadhaa wauawa

11:22 - August 09, 2022
Habari ID: 3475597
TEHRAN (IQNA)- Askari wa Jeshi la Nigeria wameshambulia kumbukuku za maomboleza ya Ashura ya Imam Hussein AS katika mji wa Zaria na kuua shahidi na kujeruhi Waislamu kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa, askari wa Nigeria jana Jumatatu waliwashambulia Waislamu hao waliokuwa katika kumbukumbu za siku ya kuuawa shahidi Imam Husain AS katika mji huo wa Zaria wa jimbo la Kaduna la kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Mmoja wa watu walioshuhudia aliyejitambulia kwa jina la Abdulhakam Muhammad amesema kuwa, Waislamu walikuwa katikati ya maombolezo ya Ashura, wakati askari wa serikali walipoanza kuwashambulia baada ya Sala ya Adhuhuri hiyo jana.

Shuhuda huyo amesema pia kuwa amemuona kwa macho yake kijana mmoja mdogo akiuawa shahidi kwa risasi za askari hao ingawa watu wengi walianza kukimbia baada ya askari wa Nigeria kuwafyatulia risasi.

Shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abu Haidar Zaria ameliambia shirika la habari la Iran Press kwamba kuna uwezekano idadi wa Waislamu waliouawa shahidi kwenye shambulio hilo wakawa ni wengi kwani polisi wamefanya haraka kuondoa majeruhi na watu waliopigwa risasi.

Kwa upande wake Sheikh Abdulhamid Bello, Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IM) inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky  amethibitisha kuwa Waislamu wanne wa Kishia waliuawa shahidi wakati askari walipovamia matembezi ya amani ya waombolezaji katika Soko Kuu la Zaria.

Maombolezo ya Siku ya Ashura hufanyika kila mwaka nchini Nigeria alkini katika miaka ya hivi karibuni maafisa wa usalama nchini humo wamekuwa wakiwashambulia na kuwaua waombolezaji.

Jana Jumatatu ilisadifiana na mwezi 10 Mfunguo Nne Muharram ambayo ni maarufu kwa jina la Siku ya Ashura ya kuuawa shahidi kikatili mjukukkuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW katika jangwa la Karbala la Iraq ya leo mwaka 61 Hijria.

Siku hii ni muhimu sana kwa Waislamu wa madhehebu ya Kishia na wapenzi wa Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad SAW kote duniani.

3480019

captcha