IQNA

Mkuu wa Idara ya Mahakama Iran

Wamagharibi wanaodai kutetea haki wameibua maafa Afrika, India, Palestina na kwingineko

18:29 - August 04, 2022
Habari ID: 3475579
TEHRAN (IQNA)- Hujjatul Islam wal Muslimin Gholamhossein Mohseni-Ejei, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, amekosoa utendakazi wa wale wanaodai kutetea haki za binadamu na kusema: Wanaodai kutetea haki za binadamu huko Magharibi hawawezi hata kueleza maana ya mwanadamu kwa njia sahihi.

Hujjatul-Islam Mohseni-Ejei, aliyasema hayo siku ya Jumanne iliyopita katika hafla ya kukabidhi tuzo ya 7 ya Haki za Binadamu za Kiislamu na Utukufu wa Mwanadamu. Mohseni-Ejei ameashiria historia ya nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu katika karne kadhaa zilizopita na kusema: Nchi hizo zimefanya jinai nyingi za kutisha katika pembe mbalimbali za dunia kwa kutumia visingizio mbalimbali; zilisababisha maafa ya kutisha huko Algeria na katika nchi nyingine za Kiafrika, India, Palestina na kadhalika, na bado zinatekeleza jinai huko Iraq na Yemen.

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema: Wavamizi wa Kizayuni walinyakua ardhi za Wapalestina wakawashikilia mateka na kuwapeleka kwenye kambi za wakimbizi. Huko Yemen wavamizi wa nchi hiyo wanaendelea kuwanyanyasa raia wanaodhulumiwa wa Yemen na kuwazingira kwa msaada wa Wamagharibi. Ameongeza kuwa: "Sambamba na hayo yote, nchi hizo zinazodai kwa uongo kuwa watetezi wa haki za binadamu zinaziweka kwenye mashinikizo makali nchi huru zinazounga mkono na kutetea haki za binadamu."

Ukosoaji wa Mohseni Ejei dhidi ya nchi zinazodai kutetea haki za binadamu za Magharibi una mashiko ya kimantiki kwa kutilia maanani rekodi mbaya za haki za binadamu ya nchi za kikoloni za Magharibi katika karne chache zilizopita, ikiwa ni pamoja na jinai zinazofanywa na Marekani kama kinara wa nchi za Magharibi katika ngazi ya kimataifa hususan mashambulizi yake dhidi ya Afghanistan na Iraq.

4075346

captcha