IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Makombora ya Israel yana uwezo wa kulenga maeneo yote ya Israel

17:28 - July 26, 2022
Habari ID: 3475541
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema makombora yenye usahihi mkubwa katika kulenga shabaha ya harakati hiyo ya muqawama yana uwezo wa kupiga sehemu yoyote ya utawala haramu wa Israel; baharini au ardhini.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya al-Mayadeen yaliyorushwa jana usiku kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 40 tangu kuasisiwa kwa harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu.

Ameeleza bayana kuwa: Visima vya gesi vya utawala wa Kizayuni wa Israel vipo ndani ya shabaha ya makombora ya Hizbullah yanayopiga kwa usahihi mkubwa.

Sayyid Nasrallah ameongeza kuwa, "Tangu mwaka 2006, adui hajawahi kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua yoyote dhidi ya Lebanon. Tel Aviv imesalia na chaguo moja tu la kufanya operesheni za kushambulia na kukimbia, ambazo hazijawa na athari yoyote kwa Lebanon."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, mwaka 1982 wakati Hizbullah ilipoanzishwa, ilikuwa harakati ya muqawama na mapambano kwa sababu ilikuwa tishio kwa Israel, lakini hii leo harakati hiyo sio tishio kwa Israel pekee, bali ni tishio kwa mradi mzima wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, taifa la Lebanon halitakubali kujidhalilisha na kujikomba kwa Marekani, na kusalimu amri kwa matakwa ya Washington ya kutaka likabidhi silaha na liutambue utawala haramu wa Israel. 

Amebainisha kuwa, "Hili si suala la Karish na Qana pekee, visima vyote vipo hatarini, hili linahusu wizi wa gesi na mafuta unaofanywa na Israel katika maji ya Palestina." Ameongeza kuwa, iwapo Lebanon itanyimwa haki yake ya kuchimba mafuta katika maeneo ya Pwani ya nchi hiyo, basi haitamruhusu yeyote kukanyaga katika maeneo yene utajiri wa mafuta na gesi ya Lebanon.

/3479845

captcha