IQNA

Bidhaa Halal

Soko linalokua la bidhaa na huduma Halal nchini Msumbiji

19:55 - June 17, 2022
Habari ID: 3475388
Tehran (IQNA)-Mauzo na matumizi ya bidhaa ‘Halal’, hasa vyakula na bidhaa za urembo, yanaongezeka nchini Msumbiji, kama ilivyo katika sehemu nyingine za dunia.

Molana Ibrahim Issa, mkurugenzi wa Tume ya Bidhaa za Halal ya Msumbiji, alisema wazalishaji nchini Msumbiji wananufaika na soko la halal la kimataifa ambalo lilikuwa dola trilioni 1.4 mwaka 2017, na inatarajiwa kukua hadi $ 2.6 trilioni ifikapo hapa 2024.

Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu (INE), asilimia 20 ya raia milioni 32.1 wa Msumbiji ni Waislamu, kutoka 17% katika sensa ya 2007.

Bidhaa au huduma‘Halal’ hutayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Tangu kuanzishwa kwa Tume ya Halal ya Msumbiji mwaka wa 2005, takriban kampuni 300 zimepokea uidhinishaji halal nchini kote, na maombi ya uidhinishaji halal yameongezeka kwa kasi kati ya 2019 na 2021, na takriban kampuni 100 zimetuma maombi. Wanachokua lesenia huanzia maduka madogo hadi maduka makubwa, mikahawa na hoteli, watengenezaji wa vyakula na vipodozi.

Ukuaji huo ulithibitishwa na Zeiss Laserda, katibu mtendaji wa Muungano wa Sekta ya Kuku wa Msumbiji, ambaye alitangaza bidhaa zote za shirika hilo kuwa "halal" katika taarifa yake. Walakini, mauzo ya kuku wa halal yamebadilika katika miaka miwili iliyopita kutokana na janga la kimataifa ya Covid-19.

Wauzaji wa reja reja pia wameona ongezeko la jumla la mauzo ya vyakula vya halal vya Msumbiji. Mkurugenzi wa bucha Talho Versalhes mjini Maputo aliiambia Salaam Gateway kuwa ongezeko la mauzo ya bidhaa za halal limesababisha kuongezeka kwa maduka yaliyoidhinishwa na sheria ya nyama nyekundu, kuku na bidhaa za nyama.

Mtazamo huu chanya ulithibitishwa na Alison J. Creasey, mtafiti wa Kimarekani katika Chuo Kikuu cha Arkansas, ambaye alisema: "Waislamu wa Msumbiji, hata wanapokuwa maskini, huwa tayari  kulipa zaidi ili kupata bidhaa zenye nembo ya ‘Halal’ kwa sababu ya imani yao.Hili lilikuwa jambo la kawaida katika eneo lenye Waislamu wengi kaskazini mwa Msumbiji.”

Kwa kujua kwamba Benki ya Dunia,  wastani wa Pato la Taifa kwa kila mwananchi wa Msumbiji, lilikuwa dola 448 mwaka 2020, na kwa msingi hiyo muelekeo huu wa kutumia bidhaa halali unaweza kuwa fursa kwa wafanyabiashara na watengenezaji.

Bidhaa nyingi zilizoidhinishwa na halali huagizwa kutoka nchi jirani za Msumbiji, hasa Afrika Kusini, Mashariki ya Kati, Asia na Ulaya, na Tume ya Halal hukagua bidhaa na duka kuhakikisha vigezo vya ‘Halal’ vinatimizwa..

Ingawa tume hiyo inasema haina takwimu za kutegemewa, inakubali kwamba uuzaji wa vipodozi ‘Halal’ nchini unawakilisha sehemu ndogo ya soko na kwamba wafanyabiashara wachache wanauza bidhaa za kutunza ngozi zenye lebo ya ‘Halal’ kama vile krimu za mikono na uso.

Naye msemaji wa Jumuiya ya Utalii ya Msumbiji alisema majadiliano na mipango ya kuanzisha vifurushi vya utalii ‘Halal’, ili kuvutia watalii wa Kiislamu kwenye fukwe kubwa nchini humo, na kuwavutia watembelee mbuga za wanyamapori na vivitio vya utamaduni wake tajiri.

Changamoto pia ni tele katika sekta ya ‘Halal’ nchini Msumbiji. Mkuu wa Kamisheni ya Halal ya Msumbiji alibainisha kuwa kanuni nchini Msumbiji hazikuwa rahisi kutekelezwa, na baadhi ya Waislamu wa Msumbiji wamelalamikia maduka makubwa huuza kuku wenye lebo ya ‘Halal’ na huchanganywa na bidhaa ambazo si ‘Halal’. Hivyo Waislamu wametakiwa kuzingatia na kupata uhakika kuhusu maduka yanayouza bidhaa ‘Halal’.

4064167

captcha