IQNA

Maandamano dhidi ya utawala wa Bahrain yafanyika London

19:37 - November 15, 2021
Habari ID: 3474560
TEHRAN (IQNA)- Maandamano yamefanyika nje ya ubalozi wa ufalme wa Bahrain mjini London Uingereza kutaka wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika gereza za ufalme huo waachiliwe huru.

Kati ya walioshiriki katika maandamano hiyo ni Ali Mushaima, mwanae katibu mkuu wa Harakati ya Haq ya Bahrain, Hassan Mushaima ambayo ni miongoni mwa wapinzani wanaoshikiliwa gerezani.

Ali amesema pia ataanza mgomo wa kususia chakula ili kuifanya jamii ya kimataifa izingatia hali ya wafungwa wa kisiasa Bahrain.

Hassan Mushaima, 73, anaugua saratani na magonjwa mengine sugu huku taarifa zikisema maafisa wa gereza wanapuuza hali yake ya kiafay. Familia yake inasema utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa utabeba dhima iwapo Mushaima ataaga dunia.

تحصن در لندن برای آزادی رهبران انقلاب بحرین

تحصن در لندن برای آزادی رهبران انقلاب بحرین

 

Mwamako wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 2011. Mwamko huu ni tofauti na harakati zingine za mwamko katika uliwengu wa Kiarabu ukiwemo mwamko uliopelekea kuangushwa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia au Husni Mubarak wa Misri. Tofauti ya mwamko wa watu wa Bahrain ni kuwa, nchi hiyo inapakana na Saudi Arabia ambayo ni mpinzani na adui mkubwa zaidi wa mwamko na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.

Kwa msingi huo, mwezi mmoja baada ya kuanza mwamko wa Februari 14, utawala wa Saudia ulituma wanajeshi wake Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza raia wa nchi hiyo. Askari hao vamizi wa Saudia waliingia Bahrain katika fremu ya 'Ngao ya Kisiwa' ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. 'Ngao ya Kisiwa' ni mapatano ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya kigeni.

Hivi sasa ukiwa ni mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain, wanajeshi wa Saudia na pia wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado wako nchini Bahrain na wanashirikiana na askari waliokodiwa wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa katika kuwakandamiza wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kupigania mageuzi hasa ya kutaka kuwepo utawala unaochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

4013378

Kishikizo: bahrain aal khalifa
captcha