Taarifa ya wizara hiyo imesema misahafu hiyo imechapishwa hivi karibuni kwa ushirikiano na Kituo cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur'ani Tukufu.
Imedokezwa kuwa mishahafu hiyo imesambazwa katika vituo 413 vya Kiislamu katika maeneo mbali mbali duniani.
Abdullatif bin Abdulaziz Al-Sheikh, Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia amesema usambazwaji misahafu hiyo ni muhimu katika kustawisha uelewa wa Qur'ani miongoni mwa vijana.