IQNA

Waghana wanawiri katika mashindano ya Qur’ani ya Morocco

20:00 - June 11, 2021
Habari ID: 3473997
TEHRAN (IQNA)-Vijana ambao waliwakilisha Ghana katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yaliyoandaliwa Morocco na Taasisi ya Mfalme Mohammad VI ya Maulamaa Waafrika wametunukiwa zawadi.

Kwa mujibu wa taarifa, vijana hao watatu wamepata zawadi ya dola elfu 2,000 kila moja kutokana na kupata nafasi nzuri katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Taasisi ya Mfalme Mohammad VI ya Maulamaa Waafrika inawaleta pamoja Maulamaa kutoka nchi 34 za Afrika na iliundwa mwaka 2015 kwa lengo la kuleta pamoja jitihada, elimu na uzoefu wa Maulamaa wa Kiislamu Afrika.

Kati ya majukumu ya taasisi hiyo ni kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani mashinani na hatimaye waliofuzu hushiriki katika fainali ya nchi zote wanachama wa taasisi hiyo.

Mwaka huu mashindano hayo yalifanyika kwa njia ya intaneti kutokana na sheria zilizowekwa katika nchi mbali mbali kuzuia kuenea corona.

3976784

captcha