Msikiti huu uko katika Mji wa Kale wa Kufa, mashariki mwa mji mtakatifu wa Najaf yapata kilomita 10 kutoka Haram Takatifu ya Imam Ali (AS).
Msikiti wa As Sahla ulijengwa na kabila la Banu Zafar, ambalo lilikuwa kabila la Ansar.
Inasemakana kuwa eneo lililo msikiti huo ni sehemu ya Ibada ya Mitume kadhaa ambao ni Ibrahim (AS), Idris (AS), Khizr (AS) na pia Maimami wa Kishia ambao ni Imam Sajjad (AS) NA Imam Sadiq (AS).