IQNA

Ongezeko la asilimia 31 la misikiti Marekani katika kipindi cha miaka 10

20:35 - June 05, 2021
Habari ID: 3473981
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya misikiti Marekani inaendelea kuongezeka ambapo mwaka 2020 kulikuwa na jumla ya misikiti 2,769 nchini humo.

“Hilo ni ongezeka la asilimia 31 kutoka mwaka 2010 wakati kulipokuwa na misikiti 2,106,” imesema ripoti iliyopewa anuani ya   “Msikiti wa Marekani 2020: Ustawi ,” ambayo imetangazwa Jumatano.

“Bila shaka, sababu kuu ya ongezko la misikiti ni ongezeko la Waislamu Marekani kutokana na wahajiri na kuzaliwa,” imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imefadhiliwa na Jumuiya ya Kiislamu Amerika Kaskazini (ISNA), Kituo cha Waislamu cha Misaada, Taasisi ya Sera ya Jamii na Ufahamu (ISPU) na Jumuiya ya Takwimu ya Asasi za Kidini Marekani (ASARB).

Ripoti hiyo pia imesema kumeshuhudiwa ongezeko la wale wanaotekeleza ibada zao misikitini.

Wanaoswali swala ya Ijumaa kwa wastani walikuwa ni 410 kila msikiti mwaka 2020 ikilinganishwa na 353 mwaka 2010 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16. Kwa ujumla asilimia 72 ya misikiti ilirekodi ongezeko la asilimia 10 la waumini wanaoshiriki Sala ya Ijumaa.

Hatahivyo ripoti hiyo imesema kumeshuhudiwa upungufu wa wanaosilimi ambapo mwaka  kwa wastani kila msikiti uliripoti watu 15.3 waliokuwa wanasilimu mwaka 2010 lakini idadi hiyo ilikuwa ni 11.3 mwaka 2020. Sababu kuu umetajwa kuwa ni kupungua idadi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wanaosilimu. Aida misikiti mingi imeongezeka zaidi katika miji mikubwa.

3474896

Kishikizo: marekani misikiti
captcha