IQNA

Imam wa Al-Azhar na Askofu Mkuu wa Canterbury wakutana kwa njia ya intaneti

10:38 - July 09, 2020
Habari ID: 3472944
TEHRAN (IQNA) – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri Sheikh Ahmed EL-Tayeb amekutana kwa njia ya intaneti na Askofu Mkuu wa Canterbury wa Kanisa la Anglikana Justin Welby ambapo wamejadili njia za kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo mbili na kustawisha mazungumzo baina yao.

Katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video, wawili hao pia walisisitiza kuwa janga la COVID-19 limeonyesha kuna haja ya hatua za pamoja na ushirikiano wakati wa maafa.

El-Tayeb amebainisha uungaji mkono wake kwa pendekezo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amependekeza usitishwaji vita katika maeneo yote ya vita na uungaji mkono wa wakimbizi walioathiriwa na janga la corona.

Welby kwa upande wake amepongeza uhusiano wa kistratijia baina ya Al-Azhar na Canterbury na kusema na kusema mazungumzo ya amani baina ya pande mbili ni yenye manufaa na yamekuwa na taathira hasa kwa vijana.

3471936

captcha