IQNA

Waziri wa Mambo ya Ndani

Waislamu ni sehemu ya jamii ya Ujerumani

10:52 - November 30, 2018
Habari ID: 3471756
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Horst Seehofer amesema Waislamu ni sehemu ya jamii ya Ujerumani.

Ameyasema hayo Jumatano mjini Berlin wakati akizungumza katika Kongamano la Nne la Uislamu nchini Ujerumani (DIK).

Matamshi hayo yamewavutia wengi kwani yanakinzana na kauli ya huko nyuma ya Seehofer ambaye alisema 'Uislamu si sehemu ya Ujerumani.'

Seehofer amebadili msimamo na kusema Waislamu wana haki na majukumu kama raia wengine wa Ujerumani na kwamba hakuna shaka kuhusu hilo.

Seehofer ni mhafidhina ambaye anatarajiwa kuachia ngazi kama kiongozi cha chama cha Kikristo cha Bavaria Christian Union (CSU).  Mwezi Machi mbali na kutoa matamshi dhidi ya Uislamu alisema msingi wa Ujerumani ni Ukristo. Alikosolewa vikali kwa matamshi hayo na amekuwa akitumia kila fursa kurekebisha kauli yake iliyojaa utata.

Kongamano Uislamu nchini Ujerumani lilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2006 na waziri wa mamabo ya ndani wakati huo Wolfgang Schäuble na huwaleta pamoja Waislamu Wajerumani na maafisa wa ngazi za juu serikalini.

Lengo la kongamano hilo ni kuimarisha ushiriki wa  Waislamu kidini na pia kuwawezesha kutengamana na jamii ya Ujerumani. Aidha kongamano hilo linalenga kuwa jukwaa la mazungumzo baina ya serikali ya jumuiya za Kiislamu. Kongamano la siku mbili la mwaka huu limejadili suala la ushawishi wa kigeni katika misikit Ujerumani na jamii za Waislamu na pia nafasi ya theolojia ya Kiislamu katika vyuo vikuu vya Ujerumani.

3467336

Kishikizo: ujerumani waislamu
captcha