Katika taarifa, kituo hicho kilichoko mjini Madina kimesema katika mwaka uliopita wa 1439 Hijria Qamaria, kilifanikiwa kusambaza nakala hizo milioni 17 ambazo zimetarjumiwa kwa lugha mbali mbali.
Taarifa hiyo imesema tokea Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha 'Malik Fahad' kifunguliwe mwaka 1405 Hijria Qamaria hadi kufikia Dhul Hijja mwaka jana, kimeweza kuchapisha nakala milioni 310 za Qur'ani Tukufu.