IQNA

Golkipa wa Misri Kombe la Dunia Akataa Zawadi ya Shirika la Pombe

21:38 - June 19, 2018
Habari ID: 3471565
TEHRAN (IQNA)- Golkipa wa Timu ya Taifa ya Soka ya Misri katika Kombe la Dunia la FIFA 2018 nchini Russia amekataa zawadi ya mchezaji bora ambayo alitunukiwa na shirika moja la utegenezaji na uuzaji pombe.

Mohamed El-Shenawy alitangazwa mshindo wa zawadi ya 'Mchezaji Bora' katika mechi ya kwanza baina ya timu yake na Uruguay Ijumaa iliyopita, lakini alikataa kupokea zawadi aliyotunukiwa.

El Shenawy, ambaye ni Muislamu mwenye kufungamana na mafundisho ya Uislamu, alikataa zawadi hiyo kwa sababu ilikuwa imetolewa na Shirika la Utegenezaji Pombe la Budweiser. Aidha kombe hilo ambalo alikuwa ametunukiwa lilikuwa  na jina na nembo ya shirika hilo la kubwa la Ujerumani la bia ambalo ni kati ya wafadhili wakuu wa kombe la dunia mwaka huu.

Kwa mujibu wa mafundisho wa Kiislamu si tu kuwa ni haramu kunywa pombe  bali pia ni haramu kutangaza, kuuza au kushajiisha utumizi wa kinywaji hicho cha kulevya.

Misri ni kati ya nchi saba za Waislamu ambazo ziko katika kombe la dunia nchini Russia zingine zikiwa ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Morocco, Tunisia, Senegal na Nigeria.

Nyota wengine Waisalmu walio katika Kombe la Dunia mwaka huu ni pamoja na Paul Pogba wa Ufaransa, Mesut Ozil wa Ujerumani na Mohammad Salah wa Misri.

3466105/

captcha