IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ndoto ya Maadui Kuhusu Mapatano ya Nyuklia ya Iran Haitotimia

21:45 - June 04, 2018
Habari ID: 3471543
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema kuwa ndoto waliyo nayo maadui kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama JCPOA kamwe haitotimia.

Amesema hayo leo katika kumbukumbu za mwaka wa 29 wa kufariki dunia Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na huku akigusia mazungumzo ya nchi za Ulaya na Iran kuhusu mapatano ya hayo ya nyuklia amesema, taifa na serikali ya Iran haiwezi kukubaliana na vikwazo vya nyuklia na kwamba njozi ya maadui kuhusu JCPOA haitaaguliwa kwamwe.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake hiyo muhimu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hatua zote zinazochukuliwa na maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu yametokana na kuchanganyikiwa na kushindwa kwao mbele ya Mfumo wa Kiislamu.

Katika hotobu hiyo aliyeoitoa leo Jumatatu mbele ya mamia ya maelfu ya watu walioshiriki katika kumbukumbu hizo zilizofanyika kwenye Haram ya Imam Khomeini MA kusini mwa Tehran, kwa mnasaba wa mwaka wa 29 wa kukumbuka siku aliyoaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei amesema, hatua hizo za maadui wa taifa la Iran huenda zikafanya ustawi wa nchi hii kwenda kwa mwendo wa taratibu, lakini katu haziwezi kuusimamisha.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa, "Tuna ufahamu kuhusu njama za maadui na tumeziweka bayana kwa watu. Maadui wa Iran wanatumia njia tatu kuu, mashinikizo ya kiuchumi, kisaikolojia na ya kivitendo dhidi ya taifa hili."

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa, lengo kuu ambalo maadui wanataka kulifikia kupitia kuiwekea vikwazo Iran na mashinikizo ya kiuchumi, ni kuwafanya wananchi wa Iran wauchukie Mfumo wao wa Kiislamu, lakini kwa wwezo wa Allah na kwa jitihada za maofisa wa serikali na wananchi wa Iran, katu maadui hawatafikia lengo hilo.

Ameongeza kuwa, Iran ilitaka kurutubisha urani kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu, lakini maadui wakaweka vizingiti ili nchi hii isifanikiwe kupata teknolojia ya nyuklia. Hata hivyo vijana wa Iran walifanikiwa kupata teknolojia hiyo licha ya njama hizo kubwa za maadui.

Huku akiashiria Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na uungaji mkono wa Iran kwa watu wanaodhulumiwa duniani, hususan wananchi wa Palestina, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa, "Kuwanga mkono watu wanaodhulumiwa ni jambo la fahari kwa Iran na nchi hii itaendelea kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa na vikosi vya muqawama, sambamba na kuunga mkono umoja na mshikamano wa nchi za eneo." 

Makumi ya maelfu ya wananchi Waislamu wa Iran wameshiriki katika maadhimisho ya mwaka wa 29 tangu afariki duni Imam Khomeini MA yaliyofanyika katika Haram yake iliyoko kusini mwa mji mkuu Tehran. Waandishi wa habari karibu 300 wa kimataifa wamefuatilia kumbukumbu hizo.

3720439

captcha