IQNA

Pendekezo la kuajiriwa Maimamu katika Jeshi la Ujerumani

15:51 - March 18, 2018
Habari ID: 3471434
TEHRAN (IQNA)- Tume wa Majeshi ya Kifederali Ujerumani, imetaka Maimamu waajiriwe katika jeshi la nchi hiyo ili kuwahudumia wanajeshi Waislamu.

Kwa mujibu wa taarifa, Hans-Peter Bartels wa Tume ya Majeshi ya Ujerumani amesema hivi sasa idadi ya Waislamu katika Jeshi la Ujerumani, ambalo ni maarufu kama Bundeswehr , ni zaidi ya 1,500. Amesema kwa msingi huo kuna haja ya kuwa na Maimamu wa kuwashughulikia katika masuala ya kidini. Hatahivyo amesema kwa sasa kuna tatizo la kuwateua Maimamu kwani wanajeshi hao ni  kutoka madhehebu mbali mbali. Amesema pamoja na hayo, amependekeza kuwa  Maimamu ambao watakaojitolea waajiriwe jeshini na wapewe mafunzo maalumu kuhusu kuamiliana na wanajeshi. Hans-Peter Bartels ameshangaa ni kwa nini baada ya kupita miaka sita tokea pendekezo la kuwaajiri Maimamu jeshini, Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani badohaijachukua maamuzi kuhusu suala hilo.

Mwezi uliopita wa Februari, Kituo cha Waislamu Ujerumani pia kilitaka Maimamu wa kuswalisha jamaa waajiriwe jeshini. Idadi ya Waisalmu Ujerumani inakadiriwa kuwa ni milioni tano kati ya watu milioni 76 nchini humo.

3700882

captcha