IQNA

Migahawa Halali inaongezeka nchini Japan

15:14 - March 18, 2018
Habari ID: 3471432
TEHRAN (IQNA) – Katika nchi za Kiislamu kwa kawaida huwa huwa hakuna tatizo kupata chakula au bidhaa halali.

Lakini Waislamu wanaosafiri katika nchi zisizo za Kiislamu hukumbwa na matatizo wakati wakitafuta chakula halali.

Hatahivyo hivi sasa kuna nchi nyingi zisizo za Kiislamu ambazo zimeweka mipango maalumu ya kuwapokea wageni au watalii Waislamu kwa kuhakikisha kuwa na hoteli na migahawa yenye kutoa huduma halali.

Nchini Japan kuna mkakati maalumu wa kuwavutia wageni Waislamu kwa kuhakikisha wanapata migahawa yenye vyakila halali katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo. Hivyo watalii wanapata fursa ya kula chakula cha Kijapani lakini ambacho ni halali.

Kuna migahwa kadhaa katika maeneo kama vile Tokyo, Chiba, Taito, Asakusa, Sano, Nikko ambayo inapika chakula cha kijapani kwa kuzingatia misingi ya chakula halali cha Kiislamu. Migahwa hiyo pia imepewa vibali vya chakula halali.

Ongezeko la watalii Waislamu katika miaka ya hivi karibuni nchini Japan limeambanatana na kuongezeka idadi ya migahwa yenye kuuza chakula halali. Hivi sasa katika viwanja vya ndege na hoteli kubwa nchini Japan kuna migahawa yenye vyakula halali. Migahawa hiyo mbali na kupika chakula halali inapika vyakula maalumu kutoka nchi za Waislamu kama vile Bangladesh, Misri, Indonesia, Iran, Malaysia, Morocco, Pakistan na Uturuki.

Aidha Waislamu wanaoishi Japan wanaweza kununua nyama halali iliyochinjwa kutoka nchi za kusini wa Asia kama vile Indonesia au Malaysia.

3465406

captcha