IQNA

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kuzingatia Qur'ani ni chimbuko la mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

11:47 - March 04, 2018
Habari ID: 3471415
TEHRAN (IQNA)-Kamanda wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Mohammad Ali Jafari amesema mafanikio ya Iran ya Kiislamu yametokana na taifa hili kuzingatia na kushikamana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Kuzingatia Qur'ani ni chimbuko la mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya IranAkihutubu katika sherehe za kufunga mashindano ya Qur'ani ya Jeshi la Kujitolea la Wananchi, Basij, mjini Tehran siku ya Jumamosi, kamanda huyo amesema mafanikio yaliyopatikana katika nyuga mbali mbali baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kutokana na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Halikadhalika amesisitiza kuwa, Jeshi la Basiji linapaswa kuwa mfano wa kuigwa na liwe ni lenye kutekeleza mafundisho ya Qur'ani katika setka mbali mbali. Amesema ili kufiukia lengo hilo kuna haja ya kuhifadhi Qur'ani na kutafakari kuhusu aya za kitabu hicho kitukufu.

Mashindano ya 25 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jeshi la Basiji yalifanyika Tehran na washindi walitunukiwa zawadi katika sherehe zilizohudhuriwa na mkamanda wa ngazi za juu wa IRGC.

3696317

captcha