IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkutano na maulamaa wa Syria

Siku ya kusali sala ya jamaa Quds Tukufu inakaribia

0:35 - March 02, 2018
Habari ID: 3471412
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, " Ni matumaini yetu sote tutaiona siku ambayo mtasali sala la jamaa mjini Quds na siku hiyo haiko mbali tena bali itafika karibuni hivi, ni sawa tu kama watu kama sisi tutakuwa bado tupo au hatupo tena".

Siku ya kusali sala ya jamaa Quds Tukufu inakaribiaAyatullah Sayyid Ali Khamenei, ameyasema hayo Alkhamisi mjini Tehran alipoonana na kundi la maulamaa wa Syria na kusisitizia wajibu wa kushikamana vilivyo na mambo yanayowaunganisha Waislamu wote. Aidha, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo  na ujumbe huo ulioongozwa na  Waziri wa Wakfu wa Syria Sheikh Dk. Mohammad Abdul-Sattar al-Sayyed kwamba, adui hawezi kufanya jeuri yoyote iwapo viongozi wa nchi na mataifa ya eneo hili watachukua maamuzi thabiti kuhusu suala la muqawama.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa Syria leo hii iko katika mstari wa mbele wa muqawama na akasema, "Ni jukumu letu kuunga mkono kusimama kidete nchi ya Syria."

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, mheshimiwa rais wa Syria Bashar al Assad amedhihirika katika sura moja ya mwana mapambano na mwana muqawama mkubwa na kwamba yupo imara na hakuna shaka yoyote kuhusu Rais al Assad; na jambo hilo ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, nchi hizi za Kiislamu tunazoziona zinaishi katika hali duni lakini si dhalili bali viongozi wake ndio madhalili. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, iwapo nchi hizo zingekuwa na viongozi wanaohisi kuwa na heshima na izza kutokana na Uislamu na utambulisho wao, basi nchi hizo zingekuwa bora kabisa na adui asingethubutu kuchukua hatua yoyote dhidi ya nchi hizo.

Akiendelea na mazungumzo yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Iran imeingia katika mwaka wa 40 wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema, tangu siku ya kwanza kabisa ya ushindi wa mapinduzi hayo matukufu, madola yote makubwa duniani yalishikamana na kuchukua hatua dhidi ya Iran. Marekani pia, vile vile Umoja wa Kisovieti, Nato na nchi karibu zote za Kiarabu na eneo hili zilikuwa pamoja na mabeberu katika hilo, hata hivyo taifa la Iran hadi leo lipo imara bali limepata maendeleo makubwa.

Akisisitiza kuhusu Umoja wa Waislamu duniani, Ayatullah Khamenei amesema, kuna haja ya kuwa na jitihada za pamoja za kukabiliana na madola ya kiistikbari ambayo yannashirikiana na Saudi Arabia katika kuibua mifarakano miongoni mwa Waislamu.

"Hatumkubali Shia anayepata himaya ya Uingereza au Sunni anayeungwa mkono na Marekani na Israel, kwa sababu Uislamu unapinga ukafiri, udhalumu na uistikbari," amesema Kiongozi Muadhamu.

Kwa upande wake, Waziri wa Waziri wa Wakfu wa Syria Sheikh Dk. Mohammad Abdul-Sattar al-Sayyed ametambua jitihada za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuongeza harakati za kupambana na uistikbari wa kimataifa. Amesema sera hiyo ya Iran imeleta mwamko na ambapo umepelekea kuwepo mikakakti ya kukomboa Quds Tukufu.

3682422

captcha