Papa Francis ameeleza kusikitishwa na mashambulizi hayo dhidi ya
Waislamu wa Rohingya wa nchini Mynamar na kusema kuwa: Watu wote
wanapaswa kusaidia ili kufanikisha kukomeshwa mashambulizi na hatua za
ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar.
Aidha amesisitiza kuhusu kusitishwa mashambulizi na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.
Waislamu karibu 100 wa kabila wa Rohingya wameuawa katika kipindi cha
siku kadhaa zilizopita wanaoishi katika mkoa wa Rakhine huko Myanmar
kufuatia kushadidi mashambulizi ya jeshi la nchi hiyo.
Waislamu wa Myanmar pia wamekuwa wakishambuliwa na Mabuddha wenye misimamo mikali
na wanajeshi wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa wa
Rakhine magharibi mwa nchi hiyo tangu miaka kadhaa iliyopita hadi sasa
yamesababisha kuuliwa na kujeruhiwa maelfu ya Waislamu hao na kuwafanya
makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. Waislamu wa Rohingya
wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka kadhaa sasa huku wakinyimwa haki zao
za msingi.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii
ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar
inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu
milioni moja na laki tatu.
Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini
Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi
za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye
misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.
3463768